Serikali imemtaka Mkandarasi kufunga taa za barabarani katika Manispaa ya Ilala kukalimisha sehemu kubwa ya mradi huo, ifikapo Januari 15, 2025 ili kuwepo mwanga wa kutosha katika maeneo ya biashara likiwemo la Kariakoo na Machinga Complex Jijjni Dar es Salaam.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa taa 21 za barabarani Ilala Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amesema kuwa, Soko la Machinga limezindua idadi hiyo ya taa, wadau watafunga taa 500 na Halmashauri itafunga na hivyo idadi ya taa zote zitakuwa 776, katika maeneo mbalimbali.
“Ni vyema Mkandarasi afanye kazi usiku na mchana, agizo la Rais Dkt. Samia lifanyiwe kazi ili mpaka kufikia Januari 15,2025, asilimia kubwa ya mradi wa ufungaji taa uwe katika hatua za mwisho kwa kuwa fedha za mradi zipo sio za kukopa mahali,” amesema Mpogolo.
Baada ya uzinduzi wa taa 21 za barabarani maeneo ya Machinga, Wafanyabiashara wameshukuru kwa kuwa kwa sasa wanaweza kufanya biashara mpaka usiku, na sehemu kubwa ya Ilala kumekuwa na mwanga na kwamba Wilaya hii ndio kubwa katika Jiji la Dar es Salaam, na ina wafanyabiashara wengi na inakusanya kodi kubwa kuliko Wilaya yoyote hapa nchini.
"Halmashauri ya Wilaya ya Ilala ina wafanyabiashara wengi kuliko zote nchini, inatakiwa kukusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 130, na hii pesa itapatikana endapo watu watafanya biashara na sio kukaa, na inakusanya pesa zaidi Halmashauri zote nchini, na pesa hizi zitapatikana endapo mazingira ya biashara na usalama vitakuwepo na kwamba, hivi vyote vitawezekana endapo tutamuombea Rais Samia maisha marefu na Afya kila mtu apige goti kumuombea," amesisitiza.
Zaidi ya asilimia 92 ya wananchi Ilala ni wafanyabiashara ambapo baada ya Soko la Kariakoo kuruhusiwa kufanya biashara saa 24, wafanyabiashara wamesema mauzo yameongezeka, biashara zinafanyika usiku na mchana na hii ni kutokana na uwezeshaji unaofanywa na Rais Samia na amewezesha Shilingi Trilioni moja katika mradi wa DMDP ambao una zaidi ya kilometa 67 ambapo Mkandarasi atafunga taa 2,214 za barabarani na taa hizi zinaenda kuongezwa katika kila barabara za Ilala.
Katika Jimbo la Ukonga barabara zenye urefu wa zaidi ya Kilometa 30 zitajengwa na kufungwa taa, ambapo pia Jimbo la Segerea barabara za Kilometa 20 zitarekebishwa na kufungwa taa.
#KhomeinTvUpdates
✍️ Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments