Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea na Mapambano dhidi ya Rushwa kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
Katika kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba mwaka 2024 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU Mkoa wa Arusha imefanya ufuatiliaji wa raslimali za Umma katika utekelezaji wa miradi 28 ya maendeleo yenye jumla ya thamani ya Tsh Bilioni 32.15.
Miradi hiyo iliyofuatiliwa ni katika Sekta ya Ujenzi, Miundombinu, Maji, Afya na Elimu ambapo baada ya kufanya ufuatiliaji, mapendekezo 63 yalitolewa huku kati ya hayo mapendekezo 36 yamefanyiwa kazi hadi kufikia Septemba 2024.
#KhomeinTvUpdates
✍️ Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments