Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeielekeza Kampuni ya Kukusanya na Kugawa Mirabaha ya Tanzania Music Rights Society (TAMRISO), kuhakikisha wanafanya mgao wa mirabaha unaotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwaka 2025 kwa makusanyo ya 2023/2024 na 2024/2025 (Julai hadi Disemba).
Maagizo hayo yametolewa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’, Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Kampuni hiyo iliyoundwa na Wasanii wa Muziki, ndiyo yenye jukumu la kukusanya na kugawa mirabaha hiyo ya Wasanii.
#KhomeinTvUpdates
✍️ Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments