RC MTWARA AWAITA WANANCHI VITUONI KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

 

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala, amewataka wakazi wa mkoa huo kutumia siku Saba za zoezi la uandikishaji wapiga kura kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, kuboresha taarifa zao na kujiandikisha upya kwa ambao hawana vitambulisho.

 

Katika kituo cha uandikishaji cha Rest House mtaa wa Shangani Mashariki, Manispaa ya Mtwara Mikindani, Mkuu wa Mkoa Kanali Patrick Sawala, akiongozana na viongozi wengine akiwemo Mkuu wa wilaya ya Mtwara Abdallah Mwaipaya na Katibu Tawala wa Mkoa huo Bahati Geuzye, wameboresha taarifa zao katika Daftari la Wapiga kura.

 


Baada ya zoezi hilo, Kanali Sawala akazungumza na waandishi wa habari, huku akitoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye vituo kuboresha taarifa zao na kujiandikisha kwa ambao hawana vitambulisho.

 


“Kwa wale ambao walikuwa hajatimiza miaka 18 na sasa wana miaka 18 au zaidi waje wapate vitambulisho vyao, na tumearifiwa kulingana na utaratibu wa Tume hata wale ambao watafikisha umri wa miaka hiyo wakati wa upigaji wa kura watakuwa wana sifa ya kupata vitambulisho.” Amesema Kanali sawala.

 

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Abdallah Mwaipaya, amewaondoa hofu wananchi wanaodhani labda watatumia muda mrefu kwenye zoezi hilo, kwa kuwaambia kuwa ni zoezi la muda mfupi, hivyo wafike kwenye vituo vya uandikishaji mapema.

 


“Kwasababu usipokuwa na hii (Kadi ya Mpiga kura) hautokuwa na sifa ya kumchagua kiongozi ambaye wewe unamtaka, kwahiyo ni vema zaidi uhakikishe kwamba unakuja kujiandikisha ili uweze kuboresha taarifa zao katika eneo ambalo wewe unaishi.”

 

Kwa upande wake, Ofisa uandikishaji wa Jimbo la Mtwara Mjini, George Mbogo, amesema “zoezi hili tunategemea litachukuwa siku Saba na uitikio mpaka sasaivi ni mkubwa kama hapa tupo kituo hiki cha Shangani East, na wananchi wamejitokeza wengi ambao wamekuja ama kujiandikisha kwa mara ya kwanza, ama kuboresha taarifa zao, ama kufuta taarifa za mtu ambaye wana taarifa zake kwamba ama alifariki au hana sifa za kupiga kura.” Amesema Mbogo.

 


Miongoni mwa wananchi waliojitokeza kituoni hapo kujiandikisha ni pamoja na Marry Kapinga, mwanafunzi wa chuo cha Ualimu Mtwara Ufundi (Mwasandube), anasema “hii ndio mara yangu ya kwanza kuja kujiandikisha kitambulisho cha upigaji wa kura, nina furaha sana na ninajihisi amani kupata na nitakapokipata hicho kitambulisho.”

 


Zoezi la uandikishaji na uboreshaji wa wananchi kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa mkoa wa Mtwara, limeanza leo Januari 28, na kutarajiwa kuhitimishwa Februari 3, 2025.

 

#KhomeinTvUpdates

 

✍️ Juma Mohamed-Mtwara

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments