Wateule wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan nao wamekuwa mstari wa mbele kuielewa falsafa ya kiutendaji ya kiongozi huyo mwenye mapenzi na wananchi wake.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko ni miongoni mwa wateule wa Rais Samia wanaotekeleza maagizo ya mkuu wa nchi kwa vitendo.
Hivi karibuni Bomboko alifanya ziara ya kikazi kwenye Kata ya Makuburi kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa eneo hilo, ambapo pamoja na mambo mengine ametoa maelekezo na maagizo mbalimbali yenye lengo la kutatua changamoto za eneo hilo.
"Nimetembelea kata ya Makuburi kusikiliza na kutatua kero za wananchi kwenye eneo lenye mgogoro kati ya wananchi na Mwekezaji, eneo ambalo linatekelezwa mradi wa ujenzi wa barabara.
"Upanuzi wa kina cha mto pamoja na ujenzi wa daraja linalounganisha upande wa Ilala na Ubungo, nimewaelekeza TARURA kufanya kikao na wananchi walioleta malalamiko ya maeneo yao kuvamiwa na kujengwa barabara na kisha kutoa upya vipimo vya barabara," amesema Bomboko.
Hatua hiyo ya Mkuu wa Wilaya imepongezwa na wananchi wa Kata hiyo.
✍️ Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments