TFS-SHAMBA LA MITI SAOHILL YASHIRIKI KAMPENI YA ‘MTI WA MAMA’

 



Ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya siku kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan, iliyofanyika 27 Januari 2025, Wakala wa Huduma za Usimamizi wa Misitu Tanzania (TFS) kupitia Shamba la Miti Saohill imeshiriki katika kampeni ya "Mti wa Mama" kwa kupanda miti katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji Mafinga iliyopo Wilayani Mufindi. 

 

Katika kampeni hiyo jumla ya miti 500 ya aina mbalimbali imepandwa katika Hospitali hiyo kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji Mafinga na wadau mbalimbali wa mazingira huku miche 400 kati ya hiyo ikitolewa na TFS. 

 

Akizungumza katika kampeni hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe.Dkt Linda Salekwa amesema kuwa kampeni hiyo imefanyika ikiwa ni kusherehekea kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa Rais na kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita katika utunzaji wa mazingira. 

 

Aidha ameipongeza TFS kwa kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi kwa wananchi na kuhamasisha upandaji miti katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Mufindi kwani imekuwa ikileta tija kubwa ikiwa ni pamoja na kuongeza upatikanaji wa malighafi na uzalishaji wa mazao ya misitu. 

 

Kampeni hiyo imeratibiwa na Kampuni ya Preshdas ambao ni wadau wa sekta ya kilimo cha miti na ufugaji nyuki na kuhudhuriwa na viongozi  kutoka Halmshauri ya Mji Mafinga akiwemo Mkurugenzi Bi Fidelisia Myovela, watumishi kutoka halmashauri na wadau mbalimbali ambapo kwa mwaka 2025 Halmashauri ya Mji Mafinga ina malengo ya kupanda takribani miti Milioni moja.

 

#KhomeinTvUpdates

 

✍️ Mwandishi wetu-Mufindi

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments