Mmoja wa vijana waliojitokeza kuwania nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Kigamboni, Dkt. Ally Mandai, Julai 1, 2025, amerejesha rasmi fomu ya kuomba kuteuliwa kupeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu ujao.
Dkt. Mandai amewasili katika ofisi za CCM Wilaya ya Kigamboni mapema asubuhi baada ya kukamilisha taratibu zote za kikatiba na za chama zinazohitajika kwa wagombea wanaotaka kushiriki mchakato wa kuomba ridhaa ya chama hicho tawala.
Hatua ya kurejesha fomu inaashiria mwanzo rasmi wa safari ya Dkt. Mandai ndani ya mchakato wa kura za maoni za CCM kupitia jimbo la Kigamboni, ambao utatumika kumpata mgombea atakayepeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments