Kamishna wa Uhifadhi Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), CPA (T) Musa Nassoro Kuji Juni 30, 2025 amekagua miradi ya maendeleo iliyopo ndani ya Hifadhi ya Taifa Mikumi akiwa katika mwendelezo wa ziara zake za kikazi katika Hifadhi za Taifa zilizopo Kanda ya Mashariki.
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na Lango la kuingilia watalii la Doma ambalo lipo mbioni kukamilika, Kituo cha kutolea taarifa kwa wageni (VIC), Mradi wa eneo la kupumzikia wageni na kula chakula cha mchana (Picnic Site), Mradi wa uwanja wa ndege wa Mikumi, Mradi wa kambi ya kulala watalii pamoja na mradi wa nyumba za kulala wageni (Bandas).
Aidha Kamishna Kuji anatarajiwa kufanya kikao na watumishi ili kupata taarifa ya utendaji kazi, changamoto na mafanikio. Aidha, pia atatoa muelekeo mpya na mikakati ya namna bora ya kuimarisha uhifadhi wa maliasili ndani ya hifadhi hiyo.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments