Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa Julai 13, 2025 amemkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Nishati, Neema Chalila Mbuja tuzo ya umahiri kufuatia mchango wake alioutoa wakati wa Maonesho ya Dunia ya Biashara ya Osaka nchini Japan kwa upande wa Mawasiliano na kuitangaza nchi.
Pongezi hizo zimetolwa wakati wa kilele cha Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu Sabasaba 2025.
Sambamba na hilo Majaliwa amempongeza Mbuja kwa kuwa muongozaji wa shughuli na kuwa mahiri wakati wa Kongamano la Kimataifa la Biashara, Uwekezaji na Utalii kwenye Maonesho ya Osaka Expo 2025.
Kwa upande wake Mbuja amemshukuru Majaliwa kwa kukabidhi tuzo hiyo iliyotolewa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara TANTRADE na kuahidi kuendelea kuitangaza Wizara ya Nishati Kimataifa.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments