Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewatakia kila la kheri wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaoendelea kujitokeza katika maeneo mbalimbali nchini kuchukua fomu za maombi ya kugombea nafasi za uongozi katika vyombo vya dola.
Katika mtandao yake ya kijamii, Rais Samia ameandika, "Ninawatakia kila la kheri wanachama wote wa chama chetu, Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaoendelea kujitokeza katika maeneo mbalimbali nchini, kuchukua fomu za maombi ya kugombea nafasi za uongozi katika vyombo vya dola.
Hatua hii ndiyo msingi wa maandalizi ya kwenda kwa wananchi, kuwaomba ridhaa ya kufanya kazi ya kuwatumikia na kushirikiana nao ili kuyafikia malengo tuliyojiwekea katika Ilani yetu."
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments