LATRA, WIZARA YA UCHUKUZI WAPATA TUZO YA UTENDAJI BORA SERIKALINI

 

Katika kuimarisha uwajibikaji na utoaji bora wa huduma kwa umma, Wizara ya Uchukuzi pamoja na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) wamepokea tuzo ya kutambua mchango wao mkubwa katika usimamizi wa sekta ya usafiri ardhini. Tuzo hiyo ilitolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Phillip Isdor Mpango, tarehe 24 Agosti 2025 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

 

LATRA imetambuliwa kama Mshindi wa Pili kati ya taasisi za Serikali zisizofanya biashara kwa kuzingatia vigezo vya utawala bora, matumizi ya mifumo ya kisasa, ubora wa huduma, kiwango cha kuridhika kwa wateja pamoja na ongezeko la wigo wa huduma. Hii ni hatua muhimu inayoonesha dhamira ya Serikali kupitia taasisi zake katika kuboresha huduma zinazotolewa kwa wananchi.

 

Kwa niaba ya Wizara ya Uchukuzi, tuzo ilipokelewa na Katibu Mkuu, Prof. Godius W. Kahyarara. Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya LATRA, Prof. Ahmed M. Ame, akiambatana na Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, CPA Habibu J. Suluo, walipokea tuzo kwa niaba ya mamlaka hiyo. Tukio hili lilifanyika kama sehemu ya kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.

 

Tuzo hiyo inaonesha jinsi taasisi hizo zinavyochangia katika kuimarisha ufanisi wa taasisi za umma kupitia matumizi ya mifumo, uwazi na uwajibikaji.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwndishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments