Watu tisa wamefariki dunia kufuatia ajali iliyotokea mapema leo desemba 26,2024 Tarakea wilayani Rombo mkoa wa Kilimanjaro ikihusisha basi la abiria la kampuni ya Ngassero lililogongana uso kwa uso na gari dogo la abiria aina ya Toyota Noah.
Kwa mujibu wa taarifa za mashuhuda kutoka eneo la ajali wameleza kuwa Basi la kampuni ya Ngassero linalofanya safari zake kati ya Tarakea na Dodoma lilikua likielekea Tarakea na gari dogo la abiria lilikua likitoka Tarakea kuelekea Moshi .
Mkuu wa wilaya ya Rombo Raymond Mangwala amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Karume iliyopo wilayani humo huku dereva wa basi la Ngassero akidaiwa kukimbia .
“ Ni kweli kumetokea ajali mbaya iliyosababisha vifo vya abiria tisa Pamoja na dereva waliokuwa kwenye gari dogo , inaonekana dereva wa gari dogo alikua akiovertake gari jingine ndipo likakutana na basi na Ngassero “ alisema Mangwala .
#KhomeinTvUpdates
✍️ Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments