Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Hamphrey Polepole aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kumuondolea hadhi ya ubalozi.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kupitia Katibu Mkuu wake, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo imeeleza kwamba imepokea barua yenye taarifa hiyo kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Moses Kusiluka.
Kwa mujibu wa barua hiyo, uamuzi huo umeanza tangu Julai 16, 2025.
Aidha, Rais Dk. Samia, kwa mamlaka aliyonayo chini ya utumishi wa umma na kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amemuachisha kazi Polepole kwa manufaa ya umma.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments