BIL. 10 KUJENGA JENGO LA HALMASHAURI RUFIJI

 

Serikali inaendelea kupeleka  maendeleo katika miji mbalimbali nchini lengo likiwa ni kuhakikisha kila Mtanzania anafikiwa na neema hizo.

 

Rufiji imefikiwa na neema hiyo na kiasi cha Shilingi Bilioni 10.6 kimeelekezwa kwenye ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Mji wa Rufiji Mkoani Pwani.

 

Tayari mkataba wa ujenzi huo umeshasainiwa na Uongozi wa Halmashauri ya Mji, tarifa ya neema hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji,  Simon Berege kwenye uzinduzi wa Tamasha la kumbukumbu ya Hayati Bibi Titi Mohamed lililofanyika hivi karibuni kwenye Viwanja vya Ujamaa Rufiji.

 

Berege amesema fedha hizo zitatumika kujenga jengo la kisasa la ghorofa tatu lenye vyumba vya ofisi 100, chumba kimoja cha huduma ya kwanza, ukumbi mmoja mkubwa wa mikutano na kumbi mbili  ndogo.

 

Jengo hilo litajengwa kwa muda wa miezi 18 na mkandarasi ni Amal Builders Ltd, kati ya fedha hizo Sh.Bilioni 9.8 ni gharama za ujenzi na sh.Milioni 800 ni kwa ajili ya Mkandarasi mshauri.

 

Aidha litakuwa na uwezo wa kubeba watumishi 300 na ni jengo la kwanza kuwa na lifti katika Wilaya ya Rufiji.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments