Spika wa Bunge Mstaafu na aliyekuwa Mbunge wa Kongwa jijini Dodoma, Job Yustino Ndugai, amefariki dunia leo Agosti 06, 2025 jijini Dodoma.
Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma cha Ofisi ya Bunge imesema “"Kwa masikitiko makubwa, naomba kutoa taarifa ya kito cha kiongozi
wetu, mwanasiasa mkongwe na Spika Mstaafu wa Bunge Mheshimiwa Job Yustino Ndugai kilichotokea leo jijini Dodoma. Natoa pole kwa familia ya Marehemu, ndugu, jamaa na Wananchi wa Jimbo la Kongwa, Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu, amesema Mheshimiwa Spika.” Imeeleza taarifa hiyo, ikimnukuu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson.
Taarifa hiyo imesema Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Kamati ya Mazishi pamoja na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa. Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi, Amina.
#KhomeinTvUpdates
✍️Juma Mohamed
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments