JKCI WAPANUA WIGO WA HUDUMA| WAFUNGUA TAWI JIPYA OYSTER PLAZA DAR

 

Serikali chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuendelea kuimarisha sekta ya afya kwa kuwajali Watanzania, imewasogezea huduma ya Vipimo na Matibabu ya Moyo, kwa kufungua Tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

 

Lengo la kufungua Tawi hilo jipya, ni kuwapa Wananchi nafasi kuwa karibu na huduma ili pale wanapopata changamoto za kiafya wasichukue muda mrefu kufuata huduma zilipo.

 

Tawi hilo lililopo katika jengo la Oyster Plaza Haile Salassie barabara ya Ali Bin Said, limeanza kutoa huduma bobezi za moyo hivi karibuni lengo likiwa kuwapa fursa wananchi kupata huduma katika maeneo tofauti na ilipo taasisi hiyo na kupunguza msongamano uliopo katika makao makuu ya Taasisi.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge, ametoa taarifa hiyo 28, Disemba Jijini Dar es Salaam.

 

Amesema, JKCI imekuwa ikiwafikia Wananchi waliopo kwa kuwafuata Mikoani na kuwapa huduma bobezi za uchunguzi na matibabu ya moyo.

 


Dkt. Kisenge amesema, JKCI pia inaendelea kuyafikia makundi ya watu mbalimbali kuwapa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo ili makundi yote yanayofikiwa yaweze kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao na kuwa na tabia za kuchunguza afya zao mara kwa mara.

 

“Tumekuwa tukiwafikia watu tofauti kuwafanyia uchunguzi wa magonjwa ya moyo, kipindi hiki cha kufunga mwaka tunatoa huduma kwa wasanii, na wanamichezo kila Jumamosi na Jumapili, katika kliniki yetu ya Kawe, Wanahabari tulishawapa huduma hii huko nyuma ila tutakuja kuwarudia tena,” amesema.

 

Nyanjura ambaye pia ni Afisa Muuguzi mbobezi wa magonjwa ya moyo amesema, katika kliniki hiyo wanatoa huduma za kliniki ya moyo, kliniki ya mishipa ya damu, kliniki ya magonjwa ya moyo kwa watoto, huduma za maabara, huduma za mazoezi kwa wagonjwa wa moyo na huduma za dharula.

#KhomeinTvUpdates

 

️ Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments