Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini LATRA imefanikiwa kurekebisha mienendo ya madereva wa mabasi makubwa ya abiria nchini, hatua iliyosaidia kupunguza ajali za barabarani kwa kiasi kikubwa.
Hayo yameainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Habib Suluo katika ofisi za VTS Mikocheni jijini Dar es Salaam, Disemba 14, 2024, baada ya kutembelewa kituoni hapo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa.
Suluo amesema kwa sasa Tanzania ni salama, wamiliki wa mabasi wanaufurahia mfumo huo na kutoa ushirikiano mzuri kwa mamlaka na ajali zimepungua sana.
Kwa upande wake Msigwa amewataka wasafirishaji hususan wale wa mabasi yaendayo mikoani kuzingatia kanuni na sheria za usafirishaji ili kuepuka ajali katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.
Pia, amewataka wasafirishaji kuepuka upandishaji wa nauli katika kipindi hiki ambacho watu wengi husafiri.
Amesema, tayari mifumo ya ukataji tiketi inaendelea kuandaliwa ili kuepuka upandishaji wa nauli kiholela unaofanywa na wasafirishaji wasio waaminifu.
Ameongeza kuwa, amefurahi kutembelea kituo hicho cha kufuatilia mfumo wa mwenendo wa magari barabarani (VTS).
Kituo cha VTS kilichopo Mikocheni, Dar es Salaam, kinasimamiwa na LATRA, ambapo katika kituo hicho kuna uwekezaji mkubwa umefanywa na serikali lengo liiiwa ni kuboresha usafirishaji.
Aidha Suluo amewasisitizia madereva na wamiliki sambamba na Watanzania wote kuhakikisha wanafuata sheria.
"Mfumo huu haupo kwa lengo la kuadhibu watu, bali ni kuhakikisha kila Mtanzania anasafiri kwa usalama, kwani maisha ya Watanzania ni muhimu, na hata mali ya mmiliki ni muhimu,
Amesisitiza pia matumizi ya 'I button', na kwa madereva ambao hawana kifaa hicho watachukuliwa hatua za kisheria.
'I button' ni kifaa maalum ambacho baada ya basi kufungwa mfumo, kifaa hicho (I button) hupatiwa dereva aliyesajiliwa na LATRA kwa jina lake na namba ya leseni yake.
Ni kifaa maalum ambacho dereva huweka kidole chake kwa ajili ya utambuzi wakati anataka kuanza safari , kwa kufanya hivyo Mamlaka kupitia mfumo maalum wa VTS inapata taarifa na kutambua dereva anayeendesha basi hilo kwa muda huo, ambapo dereva huyu kwa mujibu wa sheria za LATRA saa zake za kazi ni 8 tu ili kulinda usalama wa abiria, na iwapo atazidisha, mfumo pia unatoa taarifa na hatua kuchukuliwa.
Hii inasaidia kuondoa sintofahamu baada ya ajali, kwa kutokutambua dereva husika aliyekuwa akiendesha basi hilo.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments