MAAGIZO YA RAIS SAMIA YAENDELEA KUTEKELEZWA HATUA KWA HATUA

 

Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kutekeleza ahadi zake kwa vitendo katika nyanja mbalimbali nchini.

 

Tamanio lake la kuwahudumia wananchi ni kama pia limeeleweka mbele ya wateule wake, ambapo wengi wao wamekuwa wepesi wa kusimamia miradi ya maendeleo iliyopo katika ngazi mbalimbali za kiuongozi.

 

Miongoni mwa wateule wa Rais Samia waliofanikiwa kutosha kwenye nafasi zao ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf Kimaro ambae 

amethibitisha hilo kwa kuungana na waandishi wa habari katika kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais Samia katika suala la utunzaji wa Mazingira kwa kupanda miti.

 

Kimaro amelifanya hilo Disemba 28, 2024 kwa kushirikiana na Waandishi wa Habari na Wanamtandao wa kupinga Ukatili wa Kijinsia.

 

Pamoja na kupanda miti pia wametoa elimu kwa umma juu ya matumizi ya Nishati Safi ya kupikia ikiwa ni jitihada za kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia  katika kuhifadhi mazingira. 

 

Aidha lengo la zoezi hilo ni kutekeleza agizo la Rais Samia la kutaka kila  halmashauri nchini kuhakikisha inapanda miti 1,500,000.

 

#KhomeinTvUpdates

 

️ Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

Post a Comment

0 Comments