Siku 30 zimesalia kuelekea Mkutano Mkubwa wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika uliobeba ajenda ya upatikanaji wa haraka wa Nishati barani Afrika.
Mkutano huo muhimu kwa mustakabali wa mazingira ya Afrika unatarajiwa kufanyika Dar es Salaam, Tanzania na utahudhuriwa na Marais wa nchi mbalimbali za Afrika wakiongozwa na mwenyeji wao Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambae amebeba agenda ya Nishati Safi ya kupikia Afrika.
Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Januari 27 & 28, 2025 katika kituo cha Mikutano Mwalimu Nyerere (JNICC ).
Hii ni fursa kubwa kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo, hususani katika upande wa kiuchumi kwa wafanyabiashara wanaotoa huduma mbalimbali za kijamii.
#KhomeinTvUpdates
✍️ Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments