RAIS SAMIA ANATEKELEZA KWA VITENDO, KWAMSISI SASA WAPATA MAJI YA UHAKIKA

 

Adha ya maji katika eneo la Kwamsisi lililopo wilayani Handeni mkoani Tanga, sasa ni historia, Rais Samia Suluhu Hassan amelimaliza.

 

Hii ni baada ya kusambaa kwa video iliyoonesha wananchi wa eneo hilo wakihangaika kupata maji, mara baada ya Rais kuiona video hiyo alitoa agizo kwa Waziri wa Maji, Jumaa Awesso na kumtaka kulishughulikia haraka kero ya maji katika eneo la Komungu Kijiji cha Kwamsisi, sasa maji yamefikishwa katika kijiji hicho.  

 


Agizo la Rais Samia lilitolewa Disemba 22, 2024, ndani ya siku sita tayari utelelezaji wa agizo hilo umezaa matunda na wanakijiji wa kijiji hicho sasa wanafurahia kupata maji safi na salama.

 


Utatuzi huo wa haraka wa changamoto za wananchi unaonesha namna Rais Samia Suluhu Hassan alivyo na utayari wa kuhakikisha serikali yake inawatumikia wananchi popote walipo bila kujali eneo walipo.

 

Hii ndio maana halisi ya uongozi na Rais Samia anadhihirisha waziwazi, nia yake ya kumtumikia mwananchi kwa vitendo.

 

#KhomeinTvUpdates

 

️ Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments