RAIS SAMIA AWATAKIA HERI YA SIKUKUU WATANZANIA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anawatakia Watanzania wote kheri katika Sikukuu ya Krismasi na kuwataka kusherehekea na kujumuika na familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa furaha na upendo kama ilivyo desturi ya Watanzania. 

 

“Historia ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo itupe pia tafakari juu ya mwanzo mpya katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku, juu ya upendo kwa ndugu na jirani, juu ya uzalendo kwa Taifa letu, juu ya kuishi katika kweli, juu ya unyenyekevu tunapojaaliwa nafasi za kuwatumikia wenzetu, na juu ya shukrani,” ameandika Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

 

Pia amesisitiza Watanzania kuungana kuiombea nchi yetu iendelee kudumu katika amani, umoja na utulivu, “Mwenyezi Mungu awabariki nyote,” amemaliza Rais Samia.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments