RAIS SAMIA AZIDI KUWAVUTIA WATALII, I,160 WAINGIA NCHINI

 


Mafanikio ya jitihada za Serikali ya awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, yanaendelea kuonekana baada ya Watalii 1,160 kuja nchini kutembelea vivutio vya utalii.

 

Kuja kwa idadi hiyo kubwa ya Watalii hapa nchini, ni miongoni mwa jitihada zinazofanywa na Rais Samia katika kuhamasisha Utalii na Uwekezaji nchini, tangu alipoingia madarakani miaka mitatu iliyopita.

 

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema, huu ni Uwekezaji wa Serikali katika Sekta ya Utalii na unalipa, na kwamba tunakokutaka tutafika.

 

Msigwa ameishukuru Kampuni kubwa ya Oceania Cruises, kwa ajili ya kuleta Watalii kuja kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii hapa nchini.

 

Bodi ya Utalii (TTB), Kampuni ya Akorn na Savannah ndio zinazoongoza Watalii hao kuweza kutembelea Jijini Dar es Salaam, Pori la Akiba Pande, Hifadhi ya Taifa ya Nyerere, Bagamoyo, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Zanzibar kwa muda wa siku mbili.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments