Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia kwa Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, imemtaka mkandarasi anaejenga barabara ya Mbande- Msongola yenye urefu wa kilomita 3.8 kukamilisha kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Disemba 28, 2024, Waziri Ulega ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Akiwa kwenye ziara hiyo, Waziri Ulega amesisitiza uharaka, kasi na ubora wa utekelezaji mradi huo huku akitoa maelekezo mahususi kwa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na mkandarasi wa mradi, kampuni ya Jonec (T) Limited kutaka kuharakisha umalizaji wa mradi huo.
Akizungumza na wananchi wa Msongola, Waziri Ulega amesisitiza kuwa mkandarasi ahakikishe kazi inafanyika usiku na mchana, kuongeza wafanyakazi na vifaa, na kukamilisha ujenzi kabla ya mvua za masika.
"Wananchi wanataka kuona thamani ya fedha zao. Haiwezekani barabara ijengwe chini ya mwaka mmoja kisha iharibike. Ukijenga chini ya kiwango, utarudia kazi kwa gharama zako mwenyewe." amesema Waziri Ulega
Ziara hiyo pia iliibua ombi la wananchi la kuwekwa taa za barabarani katika eneo la Msongola Center ili kuwezesha shughuli za biashara hadi usiku na kupunguza uhalifu.
"Nataka kuona Msongola inang'aa kwa taa za barabarani, na wananchi waendelee kufanya biashara zao kwa amani na usalama hata nyakati za usiku," ameongeza Waziri Ulega.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema barabara ya Mbande - Msongola ni muhimu kwa kuunganisha wilaya za Ilala, Temeke, na Mkuranga, huku akisisitiza usimamizi wa karibu kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati.
Naye, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi John Mkumbo, amebainisha kuwa ujenzi wa barabara hiyo umefikia asilimia 50.5, na mkandarasi tayari amelipwa fedha zote.
#KhomeinTvUpdates
✍️ Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments