SERIKALI KUJENGA HOSPITALI YENYE HADHI YA MKOA UKEREWE

 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea na mkakati wake wa uboreshaji Sekta ya Afya Mkoani Mwanza, hususani ujenzi wa miundombinu katika Vituo vya Afya, sambamba na ufungaji wa vifaa vya kisasa katika vituo vya kutolea huduma hizo nchini.

 

Kufuatia jitihada hizo za Rais Samia, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amemshukuru, Rais kwa kuweka kipaumbele kujali Wananchi wake kwa uboreshaji huo, pamoja na kuhakikisha vifaa tiba vinapatikana.

 

Amebainisha hayo 27 Disemba, 2024 katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa yenye hadhi ya Mkoa itakayojengwa katika kijiji cha Bulamba, Kata ya Bukindo kwa thamani ya zaidi ya Bilioni 25.

 

Ameongeza kuwa, ndani ya muda mfupi Serikali imepeleka Mkoani humo zaidi ya Shilingi  Bilioni 49.4 kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za afya na jumla ya Trilioni 5.6 zimepokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi katika Sekta mbalimbali.

 

Aidha, amemtaka Mkandarasi pamoja na msimamizi yaani Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kutekeleza mradi huo kwa wakati kwa mujibu wa mkataba na kwa kuzingatia ubora na amewataka kuanza mara moja ujenzi kwa kuwa tayari Bilioni 6 zimeshatolewa na Serikali ambapo Mradi huo utakaotekelezwa na kampuni ya M/S DIMETOCLASA REALHOPE LIMITED kwa kipindi cha miezi 18.

 

Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Miundombinu Mkoa wa Mwanza Mhandisi Chagu Ng'oma, ameahidi kusimamia kwa dhati utekelezaji wa mradi huo ambao amefafanua kuwa awamu ya kwanza utahusisha ujenzi wa jengo kuu la hospitali litakalokuwa na uwezo wa kubeba vitanda 180, Ofisi tatu za walinzi, Jengo la kuhifadhia maiti na Jengo la umeme na kazi za nje.

 

#KhomeinTvUpdates

 

️ Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments