SERIKALI KUUPA NAFASI MCHEZO WA KRIKETI MASHULENI

 

Mchezo wa Kriketi ni moja ya michezo inayochezwa na watu wachache nchini na hasa ni Watanzania wenye asili ya India.

 

Hatua hiyo imeufanya mchezo huo kutokuwa maarufu miongoni mwa watoto wengi wa Tanzania.

 

Ukweli wa hilo umeisukuma Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kuona haja ya kuupeleka mchezo huo kwenye ngazi ya shule za msingi na sekondari nchini ili uchezwe na watu wengi zaidi.

 

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma hivi karibuni amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Chama cha Kriketi Tanzania, Dkt. B.S. Sree Kumar na kujadili namna ya  kuendeleza mchezo huo shuleni.

 

Kikao hicho kimefanyika  katika ofisi za Wizara zilizopo Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, ambapo wamejadili mpango  wa Chama cha Kriketi Tanzania  kujenga viwanja katika shule pamoja na kufanya mafunzo ya walimu wa mchezo wa Kriketi.

 

Dkt. Kumar amewasilisha ombi kwa Naibu Waziri Mwinjuma kuwa, mchezo wa Kriketi uwe miongoni mwa michezo itakayochezwa kwenye mashindano ya UMISSETA mwaka 2025.

 

Kwa upande wake Naibu Waziri ameahidi kulifanyia kazi ombi hilo na Wizara itafanya mawasiliano na Ofisi ya Rais TAMISEMI ili kuona uwezekano wa mchezo huo kuongezwa kwenye michezo ya UMISSETA.

 

#KhomeinTvUpdates

 

️ Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments