RAIS SAMIA AWEZESHA WAFANYABIASHARA KUONGEZA MAUZO SOKO LA KARIAKOO

 

Jitihada za Serikali ya awamu ya Sita, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, zimeendelea kuonekana bayana, baada ya kufanikiwa kuwezesha Wafanyabiashara katika Soko Kuu la Kariakoo Jijini Dar es Salaam, kufanya biashara saa 24, na kuwawezesha ongezeko la kipato kwa wafanyabiashara hao.

 

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto amesema, mafanikio hayo ya soko la Kariakoo kufanya biashara kwa saa 24 ni matokeo ya jitihada za Rais Samia.

 

“Wananchi wanamshukuru Rais Samia kwa kutoa fursa ya kufanya biashara saa 24, wanasema mauzo yameongezeka kwa kuwa sasa wateja wanafanya manunuzi mpaka usiku wa manane na usalama upo,”amesema Meya.

 

Amesema, hapo awali changamoto ilikuwa ni Mkandarasi kukamilisha kazi, lakini Serikali imesimamia kuhakikisha Mradi huo umekamilika na kwamba ucheleweshaji kazi wa wakandarasi ndio ilikuwa changamoto kubwa, Wakandarasi wanashinda tenda lakini hawakamilishi kazi, huyu alibakisha kazi ya karavati ya Milioni tano tu, alipoambiwa ananyang'anywa kazi, akaanza kulia kuomba apewe siku mbili, tunamshukuru Mkuu wa Wilaya ya Ilala, alipouvunja mkataba huu," amesema Meya.

 

Amewataka Wakandarasi wanaojua hawawezi kazi za Halmashauri, wasiombe kazi vinginevyo watajikuta wanapata hasara.

 

Meya Kumbilamoto amesema, mafanikio yote yanayoonekana sasa kuanzia mizigo kutoka haraka Bandarini, ujenzi wa miundombinu ya barabara na hata Mradi huu wa Soko la Kariakoo, ni jitihada za Rais Samia ambaye ndiye amewezesha Jijini la Dar es Salaam kuwa na mafanikio na muonekano mzuri.

 

 

#KhomeinTvUpdates

 

️ Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments