Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuwahudumia wananchi katika kila sekta, ambapo sasa imeelekea mkoani Ruvuma kuangalia afya ya macho kwa wananchi wake.
Kwa kuthibitisha hilo serikali imefanya uzinduzi wa kambi ya uchunguzi wa huduma bobezi ya macho, katika Mkoa wa Ruvuma inayofanyika kwa muda wa siku nne, kuanzia tarehe 26 hadi 29 Disemba 2024.
Jitihada hizo za Serikali ya Awamu ya Sita, zinalenga kujali afya za Wananchi, ikiwa ni muendelezo wa mkakati wake wa kuboresha Sekta ya Afya kwa kutoa huduma bora na muhimu hasa za Kibobezi kwa Watanzania.
Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana katika tovuti ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imeeleza kuwa, huduma hizi zinafanyika chini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Songea, ambapo uzinduzi huo wa kambi ya uchunguzi wa macho, unalengo la kutoa huduma za kibobezi kwa Wakazi wa Mkoa huo.
Huduma hii ya kambi ya uchunguzi wa macho, inayotolewa na Madaktari Bingwa, hufanywa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika Wilaya mbalimbali kila mwaka, ambapo kwa Mkoa wa Ruvuma uchunguzi wa magonjwa ya macho uliofanyika Novemba, 2023 wagonjwa 185 Mkoani Ruvuma ambapo, watu walipatiwa vipimo na matibabu ya upasuaji wa mtoto wa jicho, na mwaka huu wanatarajia kufanya upasuaji huo kwa watu 250.
#KhomeinTvUpdates
✍️ Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments