Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipanga kuwahudumia wananchi bila kuchoka kwa lengo la kuhakikisha hakuna kipingamizi katika kuyafikia maendeleo.
Katika kufanikisha hilo Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amewataka wakandarasi wa ujenzi wa njia za mabasi yanayokwenda haraka, kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ili kuukamilisha mradi huo haraka.
Katika mwanzo wa ziara yake Mkoani Dar es salaam Waziri Ulega amekagua maendeleo ya mradi wa BRT 3 Lot 1 kuanzia Mtaa wa Azikiwe, Posta ya zamani hadi Gongolamboto pamoja na mradi wa uboreshaji usalama barabarani katika mradi wa BRT 1 sehemu A kutoka Ubungo hadi Kimara na kuzungumza na wananchi.
Akizungumza na Menejimenti ya TANROADS pamoja na wataalamu wengine wanaosimamia mradi huo, aliwataka kuhakikisha kazi haisimami na inakamilika kwa wakati, hivyo njia pekee ni kufanya kazi usiku na mchana.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments