Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dk. Samia Suluhu Hassan, imetoa kiasi cha shilingi bilioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), kampasi ya Zanzibar.
Awamu ya kwanza ya ujenzi huo umeanza Septemba 2024 ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono dhamira ya serikali zote mbili za Tanzania kuhakikisha wananchi wa pande zote mbili za muungano wanafaidika na taaluma bora inayotolewa vyuo yva taasisi za elimu zilizopo nchini.
Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Profesa Willian Amos Pallangyo, alieleza hayo baada ya kukagua awamu ya kwanza ya ujenzi wa kampasi hiyo inayojengwa shehia ya Ng'anani Makunduchi, mkoa wa kusini Unguja.
Amesema ili kukamilisha ujenzi huo Serikali ya Jamuhuri ya Muungano imetoa kiasi hicho cha fedha huku serikali ya Mapinduzi Zanzibar ikitoa eneo lenye ukubwa wa hekta 56 hivyo watahakikisha wanalitendea haki eneo hilo kwa kutumia vyema fedha zilizotolewa na kukamilisha ujenzi huo kwa muda uliopangwa.
Profesa Pallangyo amesema kukamilika kwa ujenzi huo wanategemea kuwa na wanafunzi wasiopungua 1,500 watapata huduma mbali mbali zikiwemo za kumbi za mihadhara, vyumba vya maktaba, kompyuta na mabweni ya wanafunzi wa kike na kiume zaidi ya 480.
“Nimeridhika kwa hatua zilizofikiwa katika awamu ya kwanza na niahidi kulitendea haki eneo hili kwa kuhakikisha tunatunza mazingira yake na kulifanyia kazi kama ilivyokusudiwa kwani serikali imetambua sekta ya elimu na kwa sasa imekuwa ikikua zaidi”, aemeeleza Prof. Pallanyo.
Kwa upande wake, Naibu Mkuu wa chuo hicho, Mipango, Fedha na Utawala, Dk. Issaya Hassanal, amesema ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mwaka 2026 na kutoa faida za kiuchumi kwa kupokea wanafunzi kutoka Tanzania bara, Zanzibar na mataifa ya kigeni ambayo wataitumia taasisi kwa ajili ya kupata elimu.
Aidha ameongeza kuwa, ujenzi huo pia utawasaidia wananchi wa eneo hilo kupata ajira za muda na za kudumu zikiwemo za ufundi na vibarua wa ujenzi pamoja na mamantilie kupata kuuza biashara zao.
Naye, Msimamizi wa ujenzi wa mradi huo kutoka kampuni ya Salem Constructions, Muhandisi Riziki Ringo, amesema mradi huo wa miaka miwili walikabidhiwa mwezi Septemba, mwaka huu unaendelea vyema na kuahidi kuwa watatekeleza kwa wakati licha ya kuwepo kwa changamoto ndogo ndogo.
Ujenzi huo unatarajiwa kujengwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza unaoendelea hivi sasa unaohusisha mabweni ya wanafunzi na madarasa pamoja na ofisi, utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 13.5
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments