SOKO LA NAFAKA LAIMARIKA KAGERA, WAKULIMA, WAFANYABIASHARA WAMSHUKURU RAIS SAMIA

 

Wakulima na wafanyabiashara wa nafaka mkoani Kagera wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha sekta ya kilimo nchini. 

 

Hayo yamejiri hivi karibuni mkoani humo ambapo mmoja wa wafanyabiashara hao Faris Buruhani aliyewawakilisha wafanyabiashara wenzake alisema,

 

"Tunamshukuru sana Rais wetu Samia, umetuinua, bei ya nafaka hasa maharage imepanda mara dufu kutoka wastani wa Shilingi 120,000 kwa gunia la Kilo 120 mwaka 2022 na kufikia Shilingi 250,000/= hadi 350,000/= kwa mwaka huu wa 2024 ndani ya mkoa wetu wa Kagera."

 

Aidha ameongeza kuwa,haya ni mafanikio makubwa sana kiuchumi kwa wakulima wetu na sisi wajasiriamali tunaoshughulika na  nafaka.

 

Ikumbukwe pia, hivi karibuni Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa alitoa taarifa yenye neema kwa wakulima na wafanyabiashara hao kuhusiana na kusambazwa kwa ruzuku ya mbolea na mbegu bora kwa msimu wa mwaka 2024/2025,

 

Ambapo katika kipindi cha kuanzia 1 Julai, 2024 hadi kufikia 30, Novemba, 2024, jumla ya tani 253,669.342 za mbolea zenye thamani ya Shilingi 435,724,224,815 zimenunuliwa kwa utaratibu wa ruzuku na wakulima 406,966 ambapo ruzuku ya Serikali ni Shilingi 90,485,490,128.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments