Zaidi ya shilingi bilioni 6.7 zimetumika katika ujenzi wa shule za sekondari 10 katika Wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga katika kipindi cha uongozi wa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Shule hizo zimejengwa katika kata 10 kati ya 13 za wilaya hiyo ili kusogeza huduma kwa wakazi wa maeneo hayo ambao watoto wao walikuwa wanatembea umbali mrefu kwa ajili ya masomo hali iliyosababisha matokeo mabaya katika mitihani ya Elimu ya sekondari.
Hapo awali kulikuwa na kata 13 ambazo hazikuwa na shule za sekondari lakini alivyoingia madarakani Rais Dkt. Samia amepeleka fedha ambazo zimejenga shule za sekondari katika kata 10 na mwaka huu wa bajeti kuna kata nyingine ya Kwezitu imepelekewa shilingi milioni 580 kwa ajili ya kujenga shule ya sekondari na kata mbili zilizobaki Serikali inajipanga kupeleka Fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari.
Aidha Serikali inaendelea kuimarisha sekta ya elimu kwa kuendelea kutoa mafunzo kwa walimu na kuwajengea nyumba za kuishi ili waweze kufanya kazi kwa bidii na ubunifu katika sekta ya elimu.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments