Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa salamu za rambirambi kwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko kufuatia vifo vya wanafunzi saba na majeruhi 82 baada ya kupigwa na radi hivi karibuni.
Katika salamu zake hizo, Rais ameandika kwenye kurasa zake za kijamii kuwa: “Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali ya radi iliyosababisha vifo vya wanafunzi 7 na kujeruhi wengine 82 katika Shule ya Sekondari Businda, Wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita.
Natoa pole kwa Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Naibu wa Waziri Mkuu Mheshimiwa Dkt. Doto Mashaka Biteko, ndugu jamaa na marafiki kwa msiba huu.
Mwenyezi Mungu awarehemu wote waliopoteza maisha katika ajali hii, na awajalie majeruhi wote kupona kwa haraka.”
#KhomeinTvUpdates
✍️ Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments