“CCM TUMAINI THABIT KWA WATANZANIA”

 

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassani, ameendelea kuonyesha kwa vitendo ubora wa Sera za Chama Cha Mapinduzi -CCM.

 

Kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyowagusa wananchi moja kwa moja, wananchi wameonesha imani na matumaini thabit na CCM, Mkazi wa Kijiji cha Msanga mkoani Pwani, ambaye ni dereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda, Yahaya Chande amesema,

 

 "Tunamshukuru Rais Samia kwa kweli nchi inang'aa, umeme kila kona, ukienda kwetu Msanga huko Zahanati  zimejengwa, dawa zinapatikana sio lazima uje mjini, yaani siku hizi raha sana, huyu mama Mungu ambariki" amesema Chande.

 

Katika hatua nyingine Rais Samia amebainisha kuwa chama anachokiongoza kimeendelea kuwa tumaini kubwa la Watanzania.

 

Rais Samia ameyasema hayo hivi karibuni wakati chama chake kikiadhimisha miaka 48 ya kuasisiwa kwake, Februari 5,1977.

 

Katika ukurasa wake wa mtandaoni Rais Dkt. Samia amendika:

 

Kheri ya kumbukizi ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa chama chetu, Chama Cha Mapinduzi (CCM). Pongezi kwa Wanachama wetu zaidi ya milioni 12 na mamilioni ya Watanzania wanaovutiwa na sera za CCM, katika siku hii adhimu. 

 

Ahsante kwa waasisi wetu, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Karume kwa uamuzi wa kihistoria wa kuviunganisha vyama vya TANU na ASP. 

 

Tunasherehekea na kujivunia kazi kubwa iliyofanywa na waasisi wetu, huku CCM ikiendelea kuaminiwa na Watanzania, kushamiri na kutoa uongozi thabiti kwa nchi yetu. Kwa miaka 48, CCM imekuwa chama kinachounganisha watu, kuhubiri umoja, na kutekeleza ahadi zake kwa vitendo katika kuitumikia nchi yetu na watu wake. 

 

CCM inaendelea kuwa tumaini la Taifa letu na Afrika kwa ujumla. Ahadi yetu kwa Watanzania wote ni kuwa CCM imejipanga kuendelea kutoa uongozi thabiti kwa ustawi wa Taifa letu. Pamoja, tuendelee kujenga Taifa letu na kudumisha amani, udugu, upendo na utulivu.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments