JITIHADA ZA RAIS RAIS SAMIA SEKTA YA AFYA ZIMEZAA MATUNDA

 

Jitahada za Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta ya Afya zimeleta mafanikio makubwa ambapo, amesema pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano, bado kuna kazi kubwa ya kupunguza vifo vya watoto wanaozaliwa.

 

Rais Samia amesema hayo Februari 4, mwaka huu jijijini Dodoma alipokuwa akipokelewa na wakazi wa jiji hilo kutoka Dar es salaam ambako alitunukiwa tuzo ya Gates Goalkeeper.

 

Amesema taifa limepiga hatua katika kupunguza vifo vya wajawazito kutoka vifo 556 hadi vifo 104 hali kadhalika kwa upande wake watoto wenye umri chini ya miaka mitano navyo vimepungua kutokana na uwekezaji mkubwa wa serikali katika sekta ya afya.

 

Rais Samia ameeleza kuwa ili kupunguza vifo vya watoto wanaozaliwa serikali inaendelea kuwekeza katika sekta ya afya ikiwemo miundombinu, vifaa na watumishi.

 

Amebainisha kuwa, tuzo hiyo ni ushahidi kwamba dunia imetambua juhudi za Tanzania katika kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto.Tanzania ni nchi ya kwanza barani Afrika kupata tuzo ya Gates Goalkeeper.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments