NJEZA: WENYEVITI SERIKALI ZA MITAA MKATATUE KERO ZA WANANCHI

 

Wenyeviti wa serikali za mitaa waliochaguliwa katika uchaguzi mdogo mwaka jana wamehamasishwa  kutatua kero za wananchi walio waamini kuwatumikia.

 

Hatua hiyo itakuwa njia pekee ya kuleta chachu  ya  kutekeleza miradi ya  maendeleo inayo elekezwa na serikali  katika  kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan .

 


Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne Februari 18,2025 na Mbunge wa Mbeya vijijini, Oran Njeza wakati akizungumza na maelfu ya wananchi wa Kata ya Isuto wakati akiwapongeza wenyeviti wa serikali za mitaa waliochagualiwa katika uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa mwaka 2024.

 

"Niwapongeze wananchi kwa kuwachagua wenyeviti wa serikali za mitaa na vitongoji kwa kura za kishindo jambo ambalo linakwenda kuchochea shughuli za maendeleo iliyo elekezwa na Serikali ya awamu ya seta "amesema.

 


Amesema serika ya awamu ya sita imetekeleza fedha nyingi za miradi mbalimbali ya maendeleo Jimbo la Mbeya vijijini kama elimu,afya,miundombinu ya barabara na huduma ya maji.

 

Amesema uchaguzi wa serikali  za mitaa  CCM ilibuka ushindi katika vitongoji 66 kati ya 70 vya kata ya Isuto na kusisitiza kuendelea kushirikiana na viongozi na wananchi.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu-Mbeya

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments