RAIS SAMIA APELEKA KICHEKO CHA ELIMU MBEYA| AJENGA SHULE YA KISASA


 Ujenzi wa Shule ya kisasa ya Sekondari Nsalaga yenye thamani ya shilingi milioni 643 iliyopo jijini Mbeya, umepeleka kicheko kwa wakazi wa Kata ya Nsalaga.

 

Bila kupepesa macho wananchi wa Kata hiyo wamepeleka shukrani zao kwa  Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi hao kutotembea tena umbali mrefu.

 

Katika salamu za pongezi, wanafunzi wamemshukuru Rais Samia kwa kuwajali na kuwajengea shule hiyo.

 

Lakini pia wamemshukuru Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson kwa jitihada zake za kuona elimu ndani ya Jimbo lake inakuwa bora.

 

Katika kukamilisha ujenzi wa shule hiyo, Halmashauri ya jiji la Mbeya imetoa kiasi cha shilingi milioni 60 kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya Tehama na mfumo wa gesi na maji kwenye maabara.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv



Post a Comment

0 Comments