Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara, imekadiria kukusanya kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 40.2, katika mwaka wa fedha ujao wa 2025/2026, ili kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Idara ya Mipango na Uratibu wa Halmashauri hiyo, David Sinyanya, wakati akiwasilisha makadirio ya mpango wa Bajeti ya halmashauri hiyo katika kikao cha Baraza la Madiwani, kilichofanyika leo Februari 13, 2025, kikiongozwa na mwenyekiti Baisa Abdallah Baisa.
Amesema, katika makadirio hayo, fedha zilizokadiriwa kutokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ni Bilioni 7.3.
Amesema fedha nyingine ni ruzuku ya mishahara ambayo ni Bilioni 24.9, matumizi mengineyo (OC) Bilioni 2.8 na ruzuku ya wafadhili ni Bilioni 5.065.
✍️Juma Mohamed-Tandahimba
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments