CCM YAANZA RASMI SAFARI YA KUZISAKA KURA 2025 - 2030

 

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Agosti 28,2025 kimezindua kampeni zake rasmi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025. Kiongozi wa chama na mgombea Urais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameanza siku hiyo kwa kufanya dua maalum Ikulu, hii ni ishara ya hofu ya Mungu, unyenyekevu na uongozi makini.

 

Dua hiyo ikikusudia baraka, mshikamano na ushindi wa amani kwa taifa zima wakati wa kampeni. Kisha msafara wake ulielekea viwanja vya Tanganyika Packers Kawe, ambako maelfu wa wafuasi wamekusanyika.

 

Katika uzinduzi huo, Dkt. Samia na mgombea mwenza wake, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, wameeleza dira ya Ilani ya CCM 2025–2030, ikilenga maendeleo shirikishi, uchumi imara, huduma bora, na mshikamano wa kitaifa.

 

Mbio za uchaguzi zimeanza rasmi, CCM inasonga mbele kwa imani, kazi na ushindi. Ushindi hauji kwa nguvu, bali kwa neema na hekima.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwndishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments