TIMU YA DODOMA JIJI YAPATA AJALI MTO MATANDU LINDI|BASI LATUMBUKIA MTONI

 

Timu ya soka ya Dodoma Jiji ya jijini Dodoma imepata ajali leo Februari 10, 2025, baada ya Basi lao kupinduka mara Mbili kisha kutumbukia mtoni wakiwa safarini kutoka wilayani Ruangwa mkoani Lindi kuelekea jijini Dar es Salaam, ambako wanatarajia kucheza mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Simba Sc.

 


Taarifa ya msemaji wa timu hiyo Moses Mpunga, inaeleza kuwa kabla ya ajali, dereva alikita kwenye tuta ambalo limewekwa kutokana na matengenezo ya barabara ya Lindi-Dar es Salaam, katika Kijiji cha Matandu katikati ya kata ya Nangurukulu na Somanga mkoani Lindi, kabla ya baadae tairi ya mbele kupasuka kisha gari kupinduka na kutumbukia Mtoni.

 


Mpunga amesema hakuna kifo kutokana na ajali hiyo zaidi ya kuwepo kwa majeruhi ambao ni Kocha wa viungo Francis Mkanula, Mshambuliaji Rashid Mgaza na kocha wa kikosi cha U-20 aliyemtaja kwa jina moja la Rajab.

 

Amesema majeruhi hao wote wapo katika kituo cha afya cha Nangurukulu wakiendelea kupatiwa matibabu.

 

#KhomeinTvUpdates

 

✍️Juma Mohamed-Mtwara

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments