Taasisi ya Chamata Association jimbo la Mbagala wamefanya hafla ya kumuombea dua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan sambamba na ufunguzi wa ofisi, hivi karibuni Mbagala Kipati jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo iliambatana na ugawaji wa futari kwa kundi maalum la wanawake na wazee wasiojiweza.
Mwenyeiti wa Chamata Association jimbo la Mbagala Mwanaisha Kitumbi amemshukuru Rais Samia kwa utekekezaji wa miradi ya maendeleo nchini, na kusisitiza kuwa jukumu limebaki kwa Chamata kuitangaza miradi hiyo sambamba na kumuombea Rais Dkt. Samia ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mwenyekiti wa Chamata Taifa, Pendo Mwanzogela amewashukuru viongozi wa jimbo la Mbagala kwa kufanikisha hafla hiyo ambayo ina matendo ya huruma ndani yake na kulitanguliza Taifa mbele kwa kumuombea dua Rais wa Jamhuri wa Muungajo wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Vilevile amewaasa viongozi wa majimbo mengine kuiga mfano wa jimbo la Mbagala ambapo viongozi wake wamepambana na kuhakikisha wanakuwa na ofisi yao, wametanguliza maslahi ya Taifa mbele badala ya maslahi yao binafsi.
Manzongela amewasisitizia viongozi, wanachama wa Chamata na wananchi kwa ujumla kuacha tabia ya ubinafsi na kukwamisha mambo, na hata wanapokuwa katika nafasi fulani, amewaomba kuwahudumia wananchi kwa huruma na upendo bila kujivunia cheo ama nafasi walizonazo.
Aidha,wageni mbalimbali wamehudhuria hafla hiyo sambamba na viongozi wa Chamata Taifa Pendo Mwazongela, Mwenyekiti mkoa James Nkii pamoja na viongozi mbalimbali wa Chamata Association kutoka katika majimbo likiwemo jimbo la Kinondoni, na Diwani kata mbagala Kuu Mahanya Juma Mahanya.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments