Wananchi Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya wamefurahishwa na ombi la Mbunge wa Lupa, Masache Kasaka la kuomba vifaa tiba ,magari ya wagonjwa na wataalam wa afya.
Masache amewasilisha ombi hilo Aprili 26, 2025 mbele ya Waziri wa Tamisemi Mohamed Mchengerwa alipofanya ziara Wilaya ya Chunya mara baada ya kupewa nafasi ya kutoa salama za wananchi wa Jimbo la Lupa.
Masache amesema licha ya serikali kuwekeza fedha nyingi kwenye miradi ya maendeleo hususani sekta ya afya, ombi lake kwa wanachunya na kupatiwa vifaa tiba, wataalamu wa afya na magari ya wagonjwa katika vituo vya afya kikiwepo cha Sangambi.
"Mh Waziri nashukuru kwa kipindi changu cha miaka mitano kama mbunge nimefanya mambo mengi na ndio maana wana Sangambi walinichagua."amesema Masache.
Kauli hiyo ilibua shangwe kwa wananchi wilayani chunya ,huku wengine wakieleza amekuwa kimbilio na kufikika kwa wananchi.
Petro Fredy mkazi wa kijiji cha Sangambi, amesema miaka mitano ya Mbunge wao wameona jitihada za kuleta maendeleo sambamba na kuwasilisha kero za wananchi bungeni.
Katika hatua nyingine Mbunge Masache amemuomba Waziri kuitazama barabara ya kutoka Mji wa Makongorosi kujengwa kwa kiwango cha lami ili kuunganisha shughuli za kiuchumi na mikoa ya Singida na Tabora.
Kwa Upande wake, Waziri Mchengerwa aliwaeleza wanachunya kuwa anamfahamu Mbunge katika kipindi chake cha awamu tatu kuwepo serikalini hususani alipokuwa hakimu katika Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya.
"Masache namtambua tangu mimi nikiwa hakimu, na yeye alikuwa kwenye nafasi kubwa, lakini aliacha kwa ajili ya kutumikia wananchi na kuahidi kutoa Sh 300 milioni kwa kituo cha afya Sangambi.,"amesema.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu-Mbeya
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments