SERIKALI YAZIDI KUPIGA HATUA MAENDELEO YA NCHI SEKTA MBALIMBALI

 

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imezidi kutekeleza miradi ya  maendeleo katika sekta mbalimbali nchini,ikiwa ni dhamira ya Rais Samia na wateule wake, kuhakikisha uchumi wa nchi unazidi kukua.

 

Katika muktafha huo Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeendelea kusambaza umeme nchi nzima na sasa Mkoa wa Arusha umewezeshwa kupata umeme wa uhakika baada ya upanuzi wa Kituo cha kupooza na kusafirisha umeme cha Njiro, kwa kuongeza Transfoma yenye uwezo wa MVA 210 kutoka MVA 90 ya hapo awali.

 

Akizungumza na wananchi katika hafla za Sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Mkoani Arusha, mara baada ya kuzindua kituo hicho Aprili 26, 2025, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Serikali imetumia kiasi cha Shilingi Bilioni 5.2 kwa ajili ya upanuzi wa Kituo hicho ili kukiongezea Kituo uwezo kuendana na ongezeko la matumizi ya umeme.

 

“Katika ukanda huu, mahitaji ya umeme kwenye Mkoa wa Arusha ni megawati 107, Tanga Megawati 126, Manyara Megawati 14, na Kilimanjaro Megawati 68, na leo tumezindua upanuzi wa Kituo cha kupoza umeme cha Njiro, ambacho kina njia kumi za kusambaza umeme katika Mkoa wa Arusha na kuuwezesha Mkoa huu kukidhi mahitaji ya umeme kufikia Megawati 200 kulinganisha na mahitaji ya sasa ambayo ni Megawati 107” amesema Dkt. Biteko

 

Aidha DKt. Biteko amesema kuwa Serikali ipo kwenye mpango wa utekelezaji wa kufanya maboresho ya miundombinu ya umeme ikiwa ni maagizo ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha miundombinu ya umeme chakavu yote inafanyiwa ukarabati wa njia za kusafirisha umeme. 

 

“Umeme tunaweza kuwa nao kwenye uzalishaji, lakini ikawa changamoto kwenye miundombinu, ndio maana Mhe. Rais ametuagiza sasa kufanya maboresho ya miundombinu ya umeme ili tuwe na umeme wa uhakika, amesema Dkt. Biteko.

 

Ameongeza kwa kusema kuwa Wizara ya Nishati imekusudia kuhakikisha kila Mtanzania anapata kipande cha keki ya Nishati hasa Nishati ya umeme.

 

“Nilipoteuliwa niliwaambia, TANESCO hamtalala usingizi, na wote mnashuhudia kuwa hali ya umeme imebadilika sio kama miaka kumi nyuma, na TANESCO kwa kweli hawalali wanafanya kazi nzuri” amesema Dkt. Biteko.

 

Kukamilika kwa Kituo hicho kutaimarisha hali ya upatikanaji wa umeme kwenye Mikoa ya Kanda ya Kaskazini ikiwemo Mkoa wa Arusha na kuifungua kiuchumi kwa kukuza Sekta za Utalii, Viwanda na Biashara.#KhomeinTvUpdates

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments