ILANI MPYA YA CCM 2025–2030 HAIJAACHA KITU

 

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mei 30, 2025

kimezindua rasmi Ilani yake mpya ya Uchaguzi Mkuu kwa kipindi cha 2025 hadi 2030, katika Mkutano Mkuu Maalum wa Chama hicho unaofanyika jijini Dodoma kuanzia Mei 29 hadi Mei 30, 2025. Uzinduzi huo umeongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

 

Ilani hii mpya ni dira ya kisera na nyenzo ya utekelezaji wa ahadi za CCM kwa wananchi, ikiwa ni ya saba tangu Tanzania iingie katika mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992.

 

Kwa mara nyingine tena, CCM imeonesha dhamira ya dhati ya kuendeleza maendeleo jumuishi, kwa kuwasogezea wananchi huduma muhimu katika kila sekta ya maisha. Ilani hii imejikita zaidi katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli na ya kugusa maisha yao ya kila siku.

 


Baadhi ya Mambo Mahususi yaliyopangwa katika Ilani Mpya: Ukuaji wa Kilimo: Malengo ya kuongeza kasi ya ukuaji kutoka wastani wa asilimia 4.6 hadi kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.

 

Nishati Vijijini: Kila kijiji nchini kitapatiwa huduma ya umeme kabla ya mwaka 2030. Nishati Safi ya Kupikia: zaidi ya asilimia 50 ya Watanzania watumie nishati safi ya kupikia ifikapo 2030.

 

Uendelevu wa Uchumi: Kujenga uchumi imara na shindani huku deni la Taifa likibaki kuwa himilivu.

 

Afya ya Jamii: Mpango wa Kitaifa wa kuangamiza vimelea vya mbu na kuimarisha mapambano dhidi ya malaria kote nchini.

 

Ilani hii pia inasisitiza ushirikishwaji wa wananchi katika maendeleo, uboreshaji wa huduma za kijamii, na ustawi wa wananchi wote, bila kumwacha mtu nyuma.

 

Aidha, CCM inaweka msisitizo kwa matokeo ya vitendo, huku ikiahidi kuendeleza kasi ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati na kuboresha maisha ya Watanzania wote.

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments