LATRA YAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS SAMIA

 

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) inayoongozwa na mteule wa Rais Mkurugenzi CPA Habibu Suluo imeonyesha mshikamano thabiti na ajenda ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya matumizi ya Nishati Safi, katika maonyesho ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.

 

Maadhimisho hayo yanafanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete kuanzia Juni 1 hadi Juni 5, 2025, yakiwa yamebeba kauli mbiu isemayo: “Mazingira Yetu na Tanzania Ijayo, Tuwajibike Sasa: Thibiti Matumizi ya Plastiki.” Kauli mbiu hii inahamasisha kila mdau kuchukua hatua madhubuti katika kulinda mazingira kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

 

Akizungumza katika maonyesho hayo, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano LATRA, Salum Pazzy, ameeleza kuwa LATRA imechukua hatua madhubuti katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi kwenye sekta ya usafiri wa ardhini. 

 

LATRA imekuwa ikisisitiza matumizi ya vyombo vya usafiri vinavyotumia nishati safi kama vile gesi asilia na umeme, ili kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa na kuchangia katika jitihada za Kitaifa za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

 

Kwa kuunga mkono ajenda ya kitaifa ya matumizi ya nishati safi pamoja na kampeni dhidi ya plastiki, LATRA inadhihirisha dhamira ya kuijenga Tanzania yenye mifumo endelevu ya usafiri, inayolinda mazingira na kuimarisha ustawi wa jamii.

 

Maonyesho ya mwaka huu yamehudhuriwa na taasisi mbalimbali za umma na binafsi chini ya muandaaji ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, yametoa fursa kwa wadau kuonesha teknolojia na ubunifu unaosaidia kuleta suluhisho katika changamoto za kimazingira.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments