Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini Oran M. Njeza, amezitembele na kutoa mkono wa pole kwa familia za watu 29 waliofariki na majeruhi wa ajali .
Ajali hiyo ilitokea Juni 7,2025, katika mtelemko mkali wa mlima Iwambi Wilaya ya Mbeya , baada ya ya Lori lilokuwa limebeba shehena za unga kugonga magari mawili yakiwepo ya abiria.
Katika ajali hiyo watu 28 walipoteza maisha papo hapo na wengine tisa kujeruhiwa na kukimbizwa katika Hosptali Teule ya Ifisi Wilaya ya Mbeya.
Mbunge Njeza ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bajeti ya Bunge, licha ya kutoa pole amezitaka familia za majeruhi kuendelea kuwaombea.
Amesema baada ya kuwasilisha hoja za kamati bungeni jijini Dodoma Juni 16, 2025 ,amelazimika kurejea jimboni kutoa mkono wa pole kwa familia zilizo poteza wapendwa wao na kuwajulia hali majeruhi wote wa ajali hiyo.
"Nilipokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya ajali hiyo mbaya ,lakini pia nipongeze serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujitoa kushirikiana na familia za wafiwa na majeruhi.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu-Mbeya
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments