TASAC YASHIRIKI USAFI WA MAZINGIRA

 



Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeendelea kuunga mkono jitihada za Rais Samia katika suala la kuyatunza na kuyalinda Mazingira nchini, kupitia hilo TASAC limeshiriki zoezi maalum la usafi wa mazingira lililofanyika Juni 03, 2025 katika Uwanja wa Ndege jijini Dodoma. 

 

Zoezi hilo lililoshirikisha washiriki kutoka taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi, ni sehemu ya shughuli zinazofanyika katika kuadhimisha Wiki ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa inaadhimishwa mkoani Dodoma.

 

Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi zimelenga kutumia maadhimisho haya kufanya usafi wa mazingira kama kielelezo cha dhamira chanya katika kuleta mabadiliko kwenye maeneo wanayoyahudumia. 

 

Maadhimisho haya yameandaliwa na ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, ambapo Kauli mbiu ya mwaka huu  ni: “Mazingira Yetu na Tanzania Ijayo Tuwajibike Sasa, Dhibiti Matumizi ya Plastiki”.

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments