WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUFUATA MAADILI YA TAALUMA YAO

 

 Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Dkt.Malima Zacharia ambae pia ni Mratibu wa Mradi wa Year Book amewataka waandishi wa habari kuandika na kuripoti habari kwa kuzingatia maadili ya taaluma zao hasa kuelekea kipindi cha uchaguzi bila kuchagua upande wowote.

 

Malima ameyasema hayo Agosti 11 ,2025 alipokua akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari  Mkoani Mtwara yanayo husu habari za uchaguzi.

 

" Waandishi ni vyema mkazingatia maadili ya taaluma yenu ili kuandika habari ambazo zinakuwa navigezo vya kiuandishi"..Amesema Malima.

 

Kwa Upande wake Katibu wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara Bryson Mshana amewaasa waandishi wa habari kuacha kuandika habari kwa kuangalia maslahi yao binafsi na badala yake waandike kwa kufuata maslahi ya taifa. 

 


"Tuna changamoto kubwa ya waandishi wa habari na vyombo vya habari kuandika habari kwa kuangalia hatma yao wenyewe na sio hatma ya taifa,waandishi wa habari wanaandika kwaajili ya kupata nafasi za uteuzi hili jambo ni baya sio zuri kwasababu linaweza kufikisha nchi mahali pabaya."Amesema Mshana.

 

Naye Marry Mpandula mmoja kati ya washiriki wa mafunzo hayo amesema kuwa ni kipindi sahihi kwao kupata mafunzo hayo ili kuripoti habari zenye usahihi na ukweli.

 

"Mafunzo haya yamekuja wakati sahihi sana kwani itatusaidia sisi kuripoti habari sahihi na zenye ukweli ambazo hazitazua taharuki katika jamii" Amesema Marry

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Ramla Masali

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments