DKT. TULIA AKABIDHI MCHELE TANI 2 KWA WAZEE 3,000 WASIOJIWEZA

 

Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson amekabidhi mahitaji ukiwemo  mchele tani mbili kwa wazee 3,000 wanaoishi mazingira magumu katika kata 36 na mitaa 181 Jijini Mbeya.

 

DktTulia amekabidhi mahitaji hayo, Desemba 20, 2024 na kuweka bayana lengo ni kuhakikisha wazee wanaungana na watanzania kusherehekea sikukuu ya Krismas.

 


Amesema lengo lingine la msaada huo ni kuwapa tabasamu wazee na watu wenye ulemavu kuhakikisha wanaungana na watanzania wengine kusherekea sikukuu hiyo.

 

"Watanzania tujenge utamaduni wa kuwashika mkono wazee ili watabasamu kwa kutambua furaha uongeza siku za kuishi,"amesema.

 


DktTulia amefafanua kuwa awamu hii walengwa ni wale wenye hali duni ambao hawajiwezi na kubainisha katika awamu nyingine watayagusa makundi mengi.

 


"Naomba msijikie vibaya ambao hampo kwenye orodha kwani tulitoa maelekezo kwa viongozi wenu kwa walengwa tulio wahitaji ambao wamepewa mchele kilo 2 na kiasi cha Sh5,000"ameongeza.

 

Kapwile Kapwile ambaye ni mnufaika wa msaada huo, amemshukuru Dkt. Tulia na kueleza kwamba ni Mbunge wa kwanza  Jimbo la Mbeya mjini kukumbuka kundi la watu wenye uhitaji.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

Mwandishi wetu-Mbeya

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments