TANROAD MTWARA YATENGEWA BILIONI 13 MATENGENEZO YA BARABARA

 

Kwa mwaka wa fedha 2024 -2025 Wakala wa Barabara Nchini (TANROAD) mkoa wa Mtwara imetengewa bajeti kiasi cha fedha shilingi bilioni 13.670 kwa ajili ya matengenezo na bilioni 3.011 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

 

Hayo yameelezwa na Meneja wa TANROAD Mkoa wa Mtwara Dotto John disemba 20, 2024 kwenye kikao cha kwanza cha bodi ya barabara cha mwaka wa fedha 2024 -2025, Mkoani Mtwara.

 

“hadi kufikia tarehe ya kikao hiki tumefanya manunuzi ya mikataba yenye gharama za bilioni 10.273 kwa fedha za matengenezo na bilioni 2.77 kwa fedha za miradi ya maendeleo “amesema Dotto.

 

Aidha Mkoa wa Mtwara una miradi mikubwa inayoendelea kama vile barabara ya uchumi kutoka Mnivata-Tandahimba-Newala-Masasi, ambapo wakandarasi wawili wanaendelea na kazi ya ujenzi.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments