Jumla ya wagombea Sita wa kiti cha Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka vyama Sita vya Siasa wamepitishwa na Ofisi ya Katibu wa Bunge na Msimamizi wa uchaguzi kuwania kiti hicho.
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Bunge na Msimamizi wa Uchaguzi huo Baraka Leonard, imesema wagombea waliopitishwa ni Mussa Azzan Zungu kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), Veronica Charles Tyeah kutoka Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), Anitha Alfan Maya kutoka Chama cha National League for Democracy (NLD), Chrisant Nyakitita kutoka Chama cha Democratic Party
(DP), Ndonge Said Ndonge kutoka Chama cha Alliance for
Africa Farms Party (AAFP) na Amin Alfred Yango kutoka Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC).
“Hivyo, bila kuathiri Shughuli nyingine zitakazopangwa na Bunge,
tarehe 11 Novemba, 2025 saa Tatu asubuhi au muda mfupi baada ya hapo, nitawasilisha majina ya Wagombea walioteuliwa kwa Wapiga kura ambao ni Wabunge Wateule wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili Uchaguzi ufanyike kwa mujibu wa utaratibu utakaotolewa wakati wa Uchaguzi.” Imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
#KhomeinTvUpdates
✍️Juma Mohamed
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments